Ubongo unaona matatizo akili inaona fursa kwenye hayo matatizo

Share:

Listens: 0

Ni Salama

Religion & Spirituality


1 Mambo ya Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.” Nataka uone hapa anaposema walikuwa watu wenye akili za kujua nyakati na kitu cha kufanya kwenye nyakati Kwanini? Kwa sababu ukisoma kile kitabu cha Mhubiri; Mhubiri 3:1-2 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;” Mungu alipanga vitu viende kwa muda na katika huo muda kuna vitu ambavyo tunatakiwa kufanya. MFANO Mungu alipomuumba mwanadamu pamoja na umuhimu wa magari hakutuumbia magari, na kwa sababu hiyo mwanadamu alipozaliwa na kuanza kutembea huku duniani kukosekana kwa barabara hakukuwa tatizo la kimaendeleo kwa nyakati zile, ubongo ulikuwa unaona kabisa kwamba hakuna barabara na akili ilikuwa inasema huna shida nayo. Lakini ikafika mahali muda unadai vitu viende kwa speed ndipo maswali ya usafiri yakaanza kuja na ndipo vikaja vyombo vya usafiri ili kurahisisha usafirishaji na mawasiliano na kurahisisha maendeleo kwenda kwa haraka. Sasa ilipofika mahali pa namna hiyo ubongo unapoona magari halafu hauoni barabara basi wenyewe (ubongo) unasema hili ni tatizo akili inasema hii ni fursa. Kwa hiyo ukitumia ubongo bila kutumia akili utalalamika.Ukitumia ubongo na akili utatafuta majibu ya changamoto na tatizo hilo. Ukiumwa jino kwako wewe unayeumwa jino ni tatizo lakini kwa daktari ni fursa. Ukiona garage zinajengwa wameona magari yanaharibika au wanatafuta fursa. Kama akili ikiwa kazini tafsiri ya vitu vilivyoko kwenye nyakati zilizoko zinakuwa tofauti kufuatana na nyakati. Ndio maana Mungu aliwaweka wana wa isakari wenye kujua nyakati na mambo yanayotakiwa yafanyike kwenye hizo nyakati nao walikuwa 200 na walikuwa viongozi wa ndugu zao. Mtu anayeweza kufikiri kesho yako kabla kesho haijafika uwe na uhakika atakuwa kiongozi wako. Mvua inanyesha unatafuta mwamvuli zamani hakukuweko miamvuli, mvua inanyesha unatafuta mwamvuli zamani tulikuwa tunatumia majani ya migomba lakini kuna mtu akafikiri akaona jinsi ambavyo mvua ikiisha unavyohangaika kutupa lile jani akafikiri kitu cha kujifunika ili mvua ikiisha anajifunika na kila alichofikiri unakilipia. Mungu alijua kabisa ili mwanadamu aweze kuishi vizuri anahitaji masaa 8 kati ya 24 na ukilimbikiza madeni ya usingizi utakuta unakosa utulivu na macho yanashindwa kuangalia vizuri, baada ya muda utaanza kupata shida ya kula chakula, sasa kama usingizi ulikuwa wa muhimu namna hii kwanini Mungu hakutengeneza kitanda! Na ukiangalia ⅓ ya maisha ya Mwanadamu anatumia kitandani kwa hiyo hii inamaanisha ni sehemu muhimu sana. Kwanini Mungu alipotuumba asingetengeneza na kitanda ni kwa sababu alitupa akili kwamba tuamue tunalala chini au tunatengeneza kitanda ni juu yetu. Tulienda hoteli moja kule Washington DC na tulikuwa kwenye msafara wa viongozi fulani miaka kadhaa iliyopita tukapewa chumba. Tukakitazama kile chumba na kitanda chake na tukakuta vitu vimewekwa pale mezani kwa hiyo tukaamua kuvisoma tukashangaa kumbe ni button za kukusaidia unataka kulalaje! Kwetu ukitaka kulala kichwa juu unaweka mto ukitaka kulala flat unaondoa mto wenzetu wameondoa hiyo shida ni unabonyeza tu button na kitanda kina ji adjust chenyewe. Lakini uliza bei ya chumba! Ni ghali mnoo. Nilienda Canada wakati wa baridi na nilipolalamika kuna baridi wakanipeleka kwenye chumba na chumba wameki balance hali ya joto na kuna blanket linatumia umeme. Nikaona amenyanyua blanket akavuta wire akaenda kwenye soketi ya umeme akachomeka halafu akawasha umeme halafu akaniambia ingia hapo ulale nikakataa! Walipoona nimeshtuka namna hiyo yule mwenyeji wangu akaingia akajaribu akaniambia si unaona mimi sijapata shock hamna shida! nikamwambia aaa wapi! Sasa katika shida yote ile walitafuta kurahisisha maisha akili na ndio maana akili zao zimeingia kazini. Wakati wewe unalalamika baridi wao wanaishi kwa sababu akili zao zinafanya kazi. Mahali wewe unalalamika wenzio wanajikita katika kutafuta fursa.