Miscellaneous
Ametajwa na viongozi wenzake wengi kama mwanamajumuhi wa Afrika, Kutokana na utendaji wake na namna alivyokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya nchi na raia wake licha ya ukosolewaji. Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inamuangazia aliyekuwa rais wa Tanzania, hayati John Pombe Magufuli ambaye alifariki tarehe 17 ya mwezi huu akipatiwa matibabu jijini Dar es Salaam Tanzania. Mtangazaji amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, akiwa jijini Dar es Salaam, Tanzania.