Namna ya kujiandaa kukikabili kipindi hiki cha siku za mwisho (Sehemu ya pili)

Share:

Listens: 0

Ni Salama

Religion & Spirituality


Katika siku hizi za mwisho ambazo Yesu anakaribia kurudi dunia lazima ijue, mkubwa kwa mdogo lazima wajue kwamba kurudi kwa Bwana kumekaribia. Biblia inasema na watakatifu na wazidi kujitakasa, wanaofanya kazi ya Mungu na wafanye upesi maana Roho pamoja na malaika na watumishi wanasema njoo, maana yake kuna kitu kinachomzuia asije. Biblia inasema injili ya Ufalme wa Mungu itakapohubiwa kote, anasubiri tufanye kazi yake. Kama umesoma kitabu cha Luka wakati Yesu amefufuka Luka 24:44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu. Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. Matendo ya mitume inasema malaika waliokuwepo pale wakawaambia wale watu kuwa kwa jinsi wanavyomwona anaenda ndivyo watakavyomwona anarudi. Kabla ya kuwaahidi Roho Mtakatifu aliwafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Kwa sababu unaweza ukawa na Roho Mtakatifu na usielewe maandiko kwa sababu Roho Mtakatifu anahitaji ushirika wa akili, kuonyesha kwamba Roho Mtakatifu anapoingia kazini lazima akili ziwe active. Kwa sababu huko ndiko kunakoelewa. Imani inaweza kukufanya kuchukua hatua ya kitu ambacho huelewi kwa sababu huwezi kuelewa kila kitu ambacho Mungu anakuambia fanya, vingine inahitaji kuchukua hatua kwa imani, lakini pia kudumu katika hicho alichokufanyia unahitaji kudumu katika Neno kwa sababu mtu hakuitwa kuishi kwa muujiza bali kwa Neno linalotoka katika pumzi ya Mungu. Ni rahisi kuwasisitizia watu miujiza ukasahau kusisitiza kwa Neno na kwa sababu hiyo wataweka imani kwenye miujiza na kusahau Neno na watu wataanza kutafuta miujiza ilipo kila mahali badala ya kutafuta Neno lilipo, na kwa sababu hiyo hawatajifunza kutegemea Neno watajifunza kutegemea watumishi. Roho inapopokea Neno inaligeuza kuwa imani na imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, unapewa Neno na kulifuata na kufanya, saa nyingine kuna vitu vingine hata huelewi inakuaje lakini unafuata tu kwa sababu Mungu ameweka hiyo makusudi kwa sababu kuna akili zingine hazijakaa sawa kuelewa. Nilienda nchi moja inaitwa Jamhuri ya Ireland ipo kaskazini magharibi mwa nchi ya Uingereza kwenye mji wake mkuu unaitwa Dublin. Nilikuwa na vikao vya kawaida na wafadhili mbali mbali wanaofadhili nchi mbali mbali zinazoendelea na Tanzania ikiwemo. Sikuenda kuiwakilisha serikali nilienda kwa sababu ya vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yangu kufuatilia masuala ya uchumi. Kwa hiyo nikaenda kwenye hicho kikao nikawasikiliza wale wazungu kutoka mashirika na serikali mbali mbali wakieleza namna ya kuongeza misaada. Wakazungumza mipango mbali mbali juu ya nchi zinazoendelea wakati ule naenda Tanzania ulikuwa imeshapata Uhuru takribani mwaka wa 40. Wakati wao wanaongea mimi nalitazama kwa jinsi ya kibiblia, kwa hiyo nilishindwa kuvumilia nikanyosha mkono. Wakanipa nafasi ya kuongea nikawaambia ukiwa ni mzazi na una mtoto wa miaka 40 na umekuwa ukimsaidia kila wakati, na sisi kama Tanzania toka tupate uhuru mnatupa msaada tu ninyi hizi hela zenu zisizoisha mnazipata wapi?. Kwanini hamtufundishi mahali mnapata ili tusiwasumbue kila mara kuja kuomba misaada toka kwenu. Lakini hawawezi kutufundisha kwa sababu wataharibu uchumi wao. Mzungu moja ambaye tulikuwa tunashirikiana naye akaniminya kwenye suruali akaniambia Mwakasege usiseme namna hiyo, nikamwambia hapana lazima waseme hizi hela ambazo haziishi wanazipataje si watufundishe na sisi. Unaweza ukaomba kwa Mungu muujiza wa milioni moja kakupa, na unaweza kuomba kwa Mungu mbinu za kupata na mpango wa namna ya kupata milioni moja kila siku, je utataka kitu gani? (mbinu na mpango). Sasa kwa nini kukimbilia miujiza, Muujiza si mbaya maana muujiza uliwekwa kwa ajili ya Mungu kuingilia kati. Ni divine intervention, anaingilia kati kukusaidia lakini hakupanga uishi namna hiyo kwa kutegemea miujiza bali yeye ana mipango na mikakati kwa ajili yako. Ndio maana biblia haisemi kuwa najua miujiza niliyowapangia nyinyi asema Bwana, vinginevyo kila mtu angekuwa anaenda kwa Mungu kumkumbusha kuwa Mungu muujiza wangu uko wapi.