Miscellaneous
Miongoni mwa habari kuu za dunia tulizokukusanyia katika makala hii kwa juma hili utasikia kauli ya rais wa DRC Felix Tshisekedi akiomba msaada wa Ufaransa kupambana dhidi ya waasi wa ADF mashariki mwa nchi yake, lakini pia afisa wa polisi Eric Saddam akishuhudia kuhusika na mauaji ya dereva wa mwanaharakati Floribert Chebeya, Kenya kufunga kambi 2 za wakimbizi: Dadaab na Kakuma mwaka ujao, machafuko ya nchini Chad, na kasi ya maambukizi ya Corona huko India.