Miscellaneous
Umoja wa Mataifa kupitia malengo yake ya maendeleo endelevu, SDGs ya mwaka 2015 unataka vijana wapatiwe kipaumbele katika kufanikisha malengo hayo ikiwemo namba moja la kutokomeza umaskini. Serikali zinachagizwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri na ndio maana nchini Tanzania mikopo isiyo na masharti kwa vijana imekuwa mkombozi kwa vijana mkoani Mbeya ambapo takribani vijana 10 mjini Tukuyu wilaya ya Rungwe wametumia mkopo waliopatiwa kununua mashine ya kisasa ya kufyatua matofali. Awali bila mashine hiyo walifyatua matofali kati ya 300 hadi 500 kwa siku lakini sasa inatoa matofali 1000 kwa siku na zaidi ya yote wamepatiwa ajira vijana wengine. Kwa kina basi tuungane na Moses Aswile wa radio washirika Rungwe FM kutoka Tanzania.