Religion & Spirituality
UBONGO UNATAKIWA UKUSAIDIE KUWA NA MIPANGO YA KUPATA PESA LAKINI AKILI INATAKIWA ZIKUSAIDIE KUAMUA JUU YA CHANZO CHA KUPATA PESA NA KUAMUA MATUMIZI YA PESA HIZO Kazi mojawapo ya akili ni kutusaidia kupambanua mema na mabaya kwa jinsi ya Ki-Mungu ili tuweze kuchagua mema na kuacha mabaya. Biblia inatuambia kuwa akili zao kwa kutumiwa. haijasema kwa kutegemewa bali ni kutumiwa. Biblia imekataza kutegemea akili bali tunatakiwa tumtegemee Mungu. Shetani akitaka kuvuruga maisha yako atakamata akili zako maana ubongo unaweza kuwa na mipango mizuri sana ya kupata pesa lakini akili zako zisiwe vizuri katika kuangalia chanzo na matumizi ya pesa zako. Maana unaweza ukawa na mipango mizuri sana mbele ya watu au nchi lakini inaweza isikupe hela. Maana unaweza pata hasa sadaka ya shukrani ya kutoa jumapili katika hizo pesa zako. Lakini chanzo chako hakiko sawa maana kumbe hizo pesa umevunja benki mahali ukaiba. Fikiria mtu ambaye kaenda shule vizuri na kawa mhasibu mzuri na anapata mshahara mkubwa sana. Kitu cha kwanza anachofanya akiwa kazini anaanza kuiba. Sasa hapo kapata kazi kwa kutumia ubongo lakini akili zake haziko kazini na kwa sababu hiyo shetani anazitumia kumfanya aibe. Maana kama kaenda chuo na kapata cheti kwamba kasomea masuala ya accounting na Finance. Sasa badala ya kwamba kwa kuwa kasoma vizuri basi atumie ujuzi wake kuandika vizuri katika kutunza kumbu kumbu vizuri yeye anaandika asionekane kama kaiba pesa kumbe anaibia shirika au kampuni anayofanyia kazi. Lakini watu wa namna hii wanasema ni wizi wa kutumia akili. Lakini akili zimetumika vibaya na kumfanya mtu kwenda kuiba. Unahitaji kuwa na akili nzuri ambazo zinakuelekeleza kuwa hii njia ni sahihi lakini hii ni mbaya. Akili inakusaidia juu ya kutumia pesa hasa katika kuweka akiba. Mwanzo 41: 33-36 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa. Yusufu alimwambia Farao atafute mtu wa akili na hekima ili akae juu ya Misri aweze kuweka akiba kwa ajili ya kipindi cha njaa. Mithali 30: 24-25 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa joto. Chungu ni watu wasio na nguvu, sasa haina maana hawa ni watu ila inapofika katika suala la kuweka akiba wana akili kama za watu. Lakini ukweli ni kuwa chungu ni aina ya siafu au sisimizi. Katika ; Mithali 6:6-11 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha. Kuna umasikini wa kukosa akiba na si umasikini wa kukosa pesa maana watu wengi ndio wamekwama hapa. Shida yake iko kwenye akili maana Mungu kaweka akili ifanye maamuzi ya kuweka akiba. Sisimizi huwa wanakusanya chakula wakati wa hari/kiangazi ili kitumike wakati wa baridi. Kama hujakaa nchi za baridi unaweza usielewe maana unaweza fikiria baridi kama ile ya mwezi wa sita tu.Sasa ile baridi kwa msemo wa mjini tungesema hiyo ni cha mtoto. Sasa ukienda nchi za Kaskazini au kusini mwa dunia. Kuna baridi kali sana huwa inaanza mwezi October hadi Machi. Kunakuwa na baridi kali sana maana huoni hata sehemu ya ardhi hasa kama unapita na ndege isipokuwa barabara tu ambapo huwa wanakwangua. Baridi inashusha barafu sana maana inaweza shusha hadi dari ya nyumba maana ni nzito sana. Maana hata gari likiachwa nje huwa linafunikwa na barafu kabisa hadi kesho unaweza usilione maana linakuwa limefunikwa kabisa. Maana huwa wanachimba na spedi ili kuweza kulitoa gari lilipofunikwa na barafu. Sasa unaweza ukaelewa hawa wadudu wanakaa kipindi chote cha baridi wakiwa hai. kwa hiyo wanajua kuna kipindi cha kukusanya, maana wanajua kabisa hawatakiwi kula chakula chote maana wanajua kuna msimu wa njaa. Biblia inaposema hawana akida maana yake hakuna mtu wa kuwasimamia au hawana serikali ya kuilalamikia kuwa wanapita kipindi cha njaa kwa hiyo wanahitaji msaada. Wasipoweka akiba ni kwa hasara yao maana ukifika wakati wa baridi watakosa chakula na mwishowe watakufa. Watu wengi ambao hawana akiba sio kwamba hawana hela bali ni kuwa hawajui mgawanyo na kinachogawanya pesa za sasa na za kesho ni akili, sio roho. Ukitaka kukwama sasa hapo jaribu kwenda kiroho kuweka akiba, ujue lazima utakwama tu. USHUHUDA. Kuna rafiki yetu mmoja alikuwa anakula kila kitu anachopata. Alikuwa anasema siweki akiba maana sitaacha mtu hapa Duniani. Kwa hiyo alikuwa akipata kila chochote anakula kila kitu hata hatunzi akiba maana alikuwa anasema wasije watu wakagombania siku tukifa maana itakuwa shida sana. Kwa hiyo hata kama kapata zaidi basi kilichozidi alikuwa anatoa sadaka. Siku moja walipata ajali yeye na mke na watoto wao wawili wote walikufa. Huyu ndugu japo walikufa wote siku moja yaani yeye na familia yake lakini alikuwa anaishi kiroho, lakini haitakiwi uishi hivyo maana lazima ujue kuna kesho, kuna watoto watabaki kwa hiyo tumia akili yako vizuri kuweka akiba. Pia katika kuweka akiba weka akiba kwa utaratibu ambao Mungu kakupa.Wamisri walipoambiwa waweke akiba ya nafaka wao waliweka akiba za pesa na za wanyama. Sasa akiba yao iliishia baada ya muda mfupi na haikuwa na msaada kwao maana baada ya mwaka mmoja walimaliza kika kitu. Walijiuza wao na ardhi yao na haikuwa wakiwatosha. Maana bado walikuwa na miaka minne mbele na hawana kitu. Tuje kwako wewe je akiba ambayo unayo kama iko benki au mahali popote unapojua wewe, jaribu kufikiria kama huna kipato chochote kuanzia sasa na huna msaada wowote, je hiyo hela uliyonayo itakufikisha wapi? Ndipo utagundua kuwa hata mwezi humalizi ndipo utajua maisha yako yako hatarini kiasi gani. Biblia inaita umasikini wa kukosa akiba maana sio umasikini wa kukosa kipato. Shetani akitaka kukubana ili ukose akiba, atabana fikra zako wakati wa kiangazi ili usiweze kuweka akiba. Atabana akili zako uko kazini wakati huo unapata mshahara wako vizuri na unafikiri kuwa hiyo kazi haitaisha na hata wewe hukumbuki kuweka akiba. Atabana wakati biashara yako inaenda vizuri ili usikumbuke kuweka akiba wakati biashara inaingiza pesa nyingi, wewe hukumbuki hata kuweka akiba maana unajua huo mzunguko utakuwepo na kesho. Kumbuka kuwa kuna kipindi cha miaka saba ambacho kinaweza kikaja na shida, lakini wakati wa unono wa miaka saba unabanwa hata hukumbuki kuna kipindi cha njaa kinakuja. Hapo ndipo shetani anabana watu wengi sana maana unakuwa na pesa lakini unabanwa kuweka akiba. Hata ukijaribu kudunduliza unakwama kabisa. Shetani akitaka kukubana atakubana wakati una kipato kizuri usiweke akiba kwa ajili ya wakati ambao hutakuwa na kipato hicho tena.