Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Tatu)

Share:

Listens: 0

Ni Salama

Religion & Spirituality


Kwa hiyo tangu wakati ule kuna vitu ambavyo alivyokuwa anafanya moja kwa moja vinazaa tena mfano wa kile kitu alichobeba. Sasa unaweza ukaelewa kwa nini katika kipindi hiki cha Agano jipya ni lazima tuzaliwe kwa mara ya pili. Maandiko yanatuambia ndani yake tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu na Biblia inatuambia tutaishi kwa imani Ni imani ya namna gani? Waebrania anasema Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” IMANI YA KWANZA NI HII:- PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA; KWA MAANA MTU AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA AAMINI KWAMBA YEYE YUKO Yaani usiishi kama vile Mungu hayupo. Kwenye Kiswahili cha kawaida tunahiita Uchaji Kwenye tafsiri nyingine ya kiingereza inaitwa hofu ya Mungu The fear of God. Kujua ya kwamba Mungu yupo. Kwa sababu ile tu kujua ya kwamba Mungu yupo inatosha kubadilisha na kuweka msimamo wako na malengo yako kwa namna ambavyo unajua Mungu yupo. IMANI YA PILI NI HII:- KILA AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA AAMINI KWAMBA YEYE YUKO, NA KWAMBA HUWAPA THAWABU WALE WAMTAFUTAO Kwa nini tunamtafuta? kwa sababu dhambi ilitutenga naye. AINA NYINGINE YA IMANI NI KWENYE KITABU CHA Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Kwa sababu dhambi ilipoingia ilituvurugia mawasiliano yetu ya kawaida na vitu visivyoonekana na ulimwengu wa roho. Maana ilikuwa ukienda kwenye ulimwengu wa roho ni au Mungu ajifunue kwako la sivyo utakutana na ulimwengu wa roho wa ulimwengu wa giza na ndiyo maana wanadamu ni wepesi sana kushabikia vitu vya ulimwengu wa giza kuliko vile vya ulimwengu wa nuru, kwa sababu hivyo vya giza ndiyo mazingira tuliyonayo. Shetani anajiita mungu wa dunia hii na katengeneza mazingira ambayo ni kitu cha kawaida huoni watu wakishtuka watu wakienda kwenye nguvu za giza, lakini watashtuka wakisikia kwenye familia mtu akiokoka. Imani inapokuja katika Kristo Yesu au katika Neno la Mungu kazi yake mojawapo ni kukutengenezea kitu mbele yako lengo ni kitu kilichopo mbele yako ambacho unataka kukifika, na Mungu asingetaka uende na malengo yoyote unayotaka Kwa sababu Yeremia anasema Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” Tafsiri nyingine anasema “ninajua mpango niliowapangia mimi asema Bwana ni mpango wa kuwafanikisha na kuwapa tumaini katika siku zenu za usoni” Kwa hiyo Mungu analo alilokuletea duniani, huji duniani halafu unatafuta ambalo Mungu alitaka ufanye, unakuja duniani kwa sababu lipo tayari na unatakiwa ulifanye wakati huu. Na Mungu ndiye anajua. Kwa hiyo kama unataka kulijua hilo kusudi, mjue Mungu kwanza. Watu wanataka kujua Mungu alichowapa wafanye lakini hawataki kumjua Mungu. Biblia inasema mjue sana Mungu ili uwe na amani ndivyo mema yatakavyokujia Kwa hiyo kuna ile imani ya kuwa na kitu unachokitarajia, kunakuwa na malengo kwenye maisha ya kwako na hayo malengo saa hii unakuwa huyaoni kwa jinsi ya nje lakini imani inakusaidia uyaone na unakuwa na uhakika ya kwamba Mungu yupo pamoja na wewe kwa sababu siyo imani uliyoiokota mahali, bali ni imani inayotokana na Neno la Mungu kiasi ambacho kile unachokikusudia, kile unachojiwekea malengo hakiko nje ya Neno la Mungu bali kiko kwenye maisha aliyokutengenezea. Na Mungu aliweka ya kwamba Imani na Akili na Mwili vifanye kazi pamoja. Kwa lugha rahisi zaidi ni kwamba aliumba roho, nafsi na mwili vifanye kazi pamoja. Kwa hiyo katika roho Neno la Mungu likija unapokea Imani, na katika nafsi Neno la Mungu likija unapewa kuelewa ndiyo maana BIblia inasema akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko Roho haihitaji kuelewa ili kumfuata Mungu, yenyewe inahitaji kuamini na ikiisha kuamini inasonga mbele lakini akili inahitaji kuelewa, kwanini? Ili iwe na nafasi ya kuuelewesha mwili kwa sababu kufuatana na Biblia mwili hauna mpango wa kwenda mbinguni. Usifikiri ni kitu chepesi sana kwa sababu unapokuwa mtendaji wa Neno inamaanisha mpaka mwili uweze kuhusika, vinapoanza kushindana kati ya imani yako na unachofikiri na unachotaka kufanya uwe na uhakika malengo yako huwezi kuyafikia, yatabaki tu kwenye makaratasi na moyo wako maana upinzani mkubwa unaanza ndani yako na shetani anajua mahali pa kukamata ni kwenye akili. Na ndiyo maana kama unataka kumjua Mungu na kumfuata Yesu na neno lake jifunze kuombea akili zako. UHUSIANO WA KUMTUMIKIA MUNGU NA KURUDI KWA YESU (Sehemu ya Kwanza) Mathayo 24:45-51,44 “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.” Tunapozungumza juu ya kumtumikia Mungu watu wengi sana hufikiria watu wachache tu yaani wahubiri, wachungaji, wainjilisti au wanaofanya kazi kanisani. Lakini kwenye Biblia inasema kila kiungo katika mwili wa Kristo kina nafasi yake na kazi yake kwa hiyo ni mtumishi wa Mungu. Inawezekana usihubiri, lakini pale ulipo ni mtumishi wa Mungu maana yake usimame katika kusudi lake ni kueneza Ufalme wake katika kazi ufanyayo. Hakikisha watu wanamjua Mungu maana Biblia inasema kila aliye mwana anao ushuhuda haisemi kila aliye mtumishi. Lakini pia kuna watu wengine ambao wanamtumikia Mungu bila wao kujua hata Israeli aliambiwa nimekufunga mshipi ingawa hukunijua ili wapate kunijua mimi ya kwamba hakuna Mungu kama mimi Kwa hiyo wakati Mungu anamchukua Israeli ili amtumie Israeli kujifunua kwa ulimwengu, Mungu anasema Israeli hakumjua. Kwa hiyo Mungu anaweza kukutumia wakati wewe humjui kwa sababu zake yeye, anaweza kujifunua wakati anaendelea kukutumia au anaweza kunyamaza.