Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Nne)

Share:

Listens: 0

Ni Salama

Religion & Spirituality


Tunapozungumza juu ya kumtumikia Mungu watu wengi sana hufikiria watu wachache tu yaani wahubiri, wachungaji, wainjilisti au wanaofanya kazi kanisani. Lakini kwenye Biblia inasema kila kiungo katika mwili wa Kristo kina nafasi yake na kazi yake kwa hiyo ni mtumishi wa Mungu. Inawezekana usihubiri, lakini pale ulipo ni mtumishi wa Mungu maana yake usimame katika kusudi lake ni kueneza Ufalme wake katika kazi ufanyayo. Hakikisha watu wanamjua Mungu maana Biblia inasema kila aliye mwana anao ushuhuda haisemi kila aliye mtumishi. Lakini pia kuna watu wengine ambao wanamtumikia Mungu bila wao kujua hata Israeli aliambiwa nimekufunga mshipi ingawa hukunijua ili wapate kunijua mimi ya kwamba hakuna Mungu kama mimi Kwa hiyo wakati Mungu anamchukua Israeli ili amtumie Israeli kujifunua kwa ulimwengu, Mungu anasema Israeli hakumjua. Kwa hiyo Mungu anaweza kukutumia wakati wewe humjui kwa sababu zake yeye, anaweza kujifunua wakati anaendelea kukutumia au anaweza kunyamaza. Maana Yesu anasema Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, kwa hiyo kwenye jambo lolote la kumtumikia Mungu, kwenye jambo lolote la kuishi hapa duniani, kati ya lengo mojawapo ambalo Mungu anategemea kila mtu awe nalo liwe ni lengo la kukutana na Yesu na kuishi naye milele Hivyo ni muhimu sana kuzungumza na waliokuzunguka kwa habari ya maisha yao na Yesu kabla ya kuondoka hapa duniani ndivyo Wathesalonike inavyotuambia 1 Wathesalonike 4:13-16 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.” 1 Wathesalonike 5:1-2 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.” 1 Mambo ya Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.” Anazungumzia juu ya kurudi kwa Yesu na maandiko yanasema kwa sababu hatujui siku wala saa basi tujiweke tayari, yaani tukae mkao wa kuwa tayari wakati wote.