Religion & Spirituality
Kama huna uhakika Yesu akikuita muda huu huna uhakika hakikisha leo unaokoka Wakati fulani tulisafiri na mzungu mmoja alikuwa ni mjerumani toka Arusha kwenda Dar es salaam. Aliombewa lift na mwenzake ili tusafiri naye, tukamuuliza je umeokoka akasema hapana. Yeye anamuabudu shetani na anatoka kanisa linalomuabudu shetani. Nikamwambia hamna kanisa la namna hiyo. Nikamuuliza alikuwa anasali kanisa gani akanitajia kanisa la Kikristo alilokuwa anaabudu kabla ya kuacha. Tukamuuliza tena kwa nini uliacha kwenda kanisani? Na akasema kanisa ni “very boaring” na kumepoa sana kanisani. Alisema huwa wanamtaja Mungu na sijawahi kumuona kanisani, lakini shetani anapojatwa huwa namuona. Wakati huo nilikiwa naendesha gari, nikamuuliza tena kuwa hapa tukipata ajali tukafa je utaenda wapi? akasema sijui. Nikamwambia sisi tukifa hapa tunaenda mbinguni. Nikamwambia huko ulikoenda siyo kuzuri maana walitakiwa kukueleza kuwa utaenda wapi baada ya dunia hii. Tulipofika Mombo nikawa naendesha gari huku naomba na kuangusha ngome katika akili yake. Baada ya hapo nikamwambia kuwa ukiwa tayari kama unataka kumpa Yesu maisha ili ukifa leo uende mbinguni utaniambia nisimamishe gari. Nikaendelea kuombea akili zake. Basi tulipofika Korogwe akasema Mwakasege simamisha gari namtaka huyu Yesu unayemsema. Nikapaki pembeni nikamuongoza sala ya Toba. Sasa nikamuuliza kuwa unaenda wapi? Akasema anaenda Zimbabwe. Maana nilijiuliza kuwa kwanini atoke Arusha asafiri kwa gari hadi Dar es Salaam halafu atafute ndege ndipo aende Zimbabwe?. Kama si Mungu kumpangia maana kamkimbia Yesu Ujerumani na kakamatiwa Tanzania. AMBA ZA SADAKA NA MAOMBI ?? https://goo.gl/7XcFiP MAOMBI YA KUOKOKA NA KITABU CHA HONGERA KWA KUOKOKA. ?? https://goo.gl/XKoJNB