Miscellaneous
Miongoni mwa yaliyomo Leah Mushi amefanya mazungumzo na Dokta. Paul Mutungi Afisa wa mashinani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO akihusika na wafugaji katika Ukanda wa Afrika wakiangazia suala la ukame na njaa kali unavyoathiri wananchi walioko Afrika Mashariki na pembe ya Afrika. Mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi kwa mwaka huu wa 2022 yameng’oa nanga hii leo huko Beijing China huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akitoa wito wa mshikamano wakati wa michezo na hata baada. Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Madagascar na washirika wake wengine wa misaada ya kibinadamu wanaongeza juhudi za kujitayarisha na Kimbunga Batsirai ambacho kinatarajiwa kuipinga nchi ya Madagascar mwishoni mwa wiki hii. Ikiwa leo ni siku ya saratani duniani, mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo la nishati ya atomiki, IAEA, na afya duniani WHO yamezindua programu iitwayo Rays of Hope, au ‘Miale ya Matumaini’ kwa ajili ya kuwezesha nchi wanachama hususan za kipato cha chini na cha kati. Na leo katika neno la Wiki tunakwenda Tanzania, kupata ufafanuzi wa msemo "HIARI YASHINDA UTUMWA" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla.