Miscellaneous
Miongoni mwa tuliyonano kutoka UN Leo ni mara ya kwanza kuadhimishwa kwa siku ya kimataifa ya maeneo oevu tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio mwezi Agosti mwaka jana 2021. Tunabisha hodi nchini Laos kuona harakati za kuhifadhi maeneo hayo adhimu. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limelaani vikali mauaji ya watoto 15 katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO wametaka hatua ziwekwe kulinda afya ya wafanyakazi wakati wa kufanya kazi kutokea nyumbani. Na mashinani tutausikia ujumbe na wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu msimamo wa UN kwa mapinduzi ya kijeshi ambayo yameonekana kushika kasi katika siku za hivi karibuni.